Our Blog

[THEME] 1 Thessalonians 5:23b,
May your whole Soul, Body and Spirit be kept blameless at the coming of our Lord Jesus Christ.

Tuesday, 16 January 2018 21:42

UREJESHO KATIKA UAMINIFU

Written by
Rate this item
(0 votes)

Neno uminifu linapotajwa nakutua kwenye sikio, mara nyingi litazamisha fikra za teneja kwenye uhusiano baina yake na yule mwenye jinsia tofauti naye. Hilo halitatufaa kwa sasa. Uaminifu waafaa kudhihirika kwenye nyanja zote za maisha ; baina ya wanadamu wenyewe na baina ya wanadamu na muumba wao.

Uaminifu wetu kwa mwenyezi Mungu unajitokeza wazi katika huduma zetu kwa wezetu au kanisa,katika mitihani yetu, katika kutetea na kudhibitisha ukristo wetu. Katika ahadi zilizoko baina yetu na mwenyezi mungu, katika nyanja za haki na sheria na hatimaye katika uongozi wa ngazi zozote zile.

Kila aishiye awe mwaminifu kwa maana mungu wetu ni mwaminifu kila siku. Kwa mfano; siku moja jumapili tarehe kumi na tisa mwezi Juni mwaka huu mwendo wa saa saba mchana, nilinusurika kifo kutokana na ajali iliyohusisha trela na gari la abiria. Kwa kweli niliuona uaminifu wa mungu kwa maana mungu ndiye alipelekea kuchelewa kwangu kufika palipotokea ile ajali kwa sekunde sita pekee. Hapo nilikumbumba dua langu kwa mwenyezi mungu kila siku anipe maisha marefu niifanye kazi yake.

Kulingana na hali ilivyo duniani,uhaminifu wetu wanadamu kwa muumba wetu haupo. Hili linadhihirika katika nyanja mbalimbali maishani mwetu. Tunawalizi na wasimamizi wakali katika vyumba vyetu vya mitihani kwa maana sisi sio waaminifu tena. Katika makampuni na vyumba vya kifahari vina kamera za kunasa watu na shughuli zao kwa sababu uaminifu haupo tena.

Kutoaminiana kumekosanisha familia, marafiki na hata wapenzi thibitisho tosha kuwa dunia sio pahali salama tena pa kuisha. Mungu wetu ni wa msamaha na wa urejesho. Ni kwa kuchangua kwetu tumrejee na kudumisha uaminifu wetu naye.

Mathayo 7:8, “Kwa maana kila oambaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”
Read 292 times Last modified on Tuesday, 16 January 2018 21:48
Administrator

Dear Visitor, we value you feedback as the Christian Union because it will enable us to grow in one way or another. You may therefore leave a comment any time you wish after reading through our articles and God will bless you! As the Christian body,our desire is to encourage everyone, share the biblical message that Jesus Christ is the risen Son of God, that He loves each person unconditionally, and that He desires a personal, one-on-one relationship with every man, woman, and child

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Slider